Hadithi Tukufu za Bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w) na Maiman watwaharifu (a.s)

E-mail Print PDF

AINA ZA AHADITH

Sayyid Ibn Taus a.r. (amefariki 673 Hijriyyah) na ‘Allamaha Hilli a.r. (amefariki 726 Hijriyyah) kwa juhudi zao, wao wamefanikiwa kutuletea kanuni nne kuu zijulikanazo usul-i-‘arbi’ah ambazo ni kama zifuatazo:

1. HADITH SAHIH

 

 

Rawi wote lazima wawe waaminifu na Shia Ithna-Asheri na riwaya hizo ziwe zikifika hadi kwa Ma’sumiin a.s.

2. HADITH HASAN

Riwaya ambazo Rawi wake ni Mashiah na ambapo hapakufanywa uchunguzi wowote juu ya uadilifu wao.

Hadith kama hizo zinajulikana kama hasan kwa sababu Rawi amepokelewa kwa misingi ya husn-dhan yaani kwa dhana njema.

3. MUTAWATH-THAQ

Yaani Rawi wote wawe wakiaminiwa lakini miongoni mwao si wote ambao ni Mashiah.

4. DHAIF

Ni riwaya zile ambazo hazina sifa hata mojawapo za hapo juu.Tanbih lipo jambo moja la kuzingatia, kuwa Ma’ulamaa wanakubaliana na Hadith zilizo Sahih, Hasan na Muwath-thiq.

Ama kuhusu Hadith zilizo dhaif ni kwamba iwapo atayumkinika kuwa Rawi hao si watu wa kutegemewa lakini maelezo na maana yake ni sawa na maana ile ya Ma’sumiin (a.s), katika sura hii, (hadithi hizo)zitaweza kukubalika, na wakati Ma’ulamaa wanaozisimulia basi nia yao huwa juu ya Hadith, bali huwa ni kutoa ushahidi tu.

HADITH ZILIZOTOLEWA

Kwa mujibu wa kanuni hizi nne, mmefahamu kuwa Hadithinapoangukia kuwa dhaifu haimaanishi kuwa ni Hadith ya uongo, yenye mfululizo dhaifu, na kwa dalili zinginezo na kwa nyenzo zinginezo inaweza kuthibitika kuwa Hadith hiyo inaweza kukubalika, Lakini inapokuwa imekosewa kabisa basi huitwa Kidhb (uongo) au Iftira’ (tuhuma).

Yaani utaratibu uliotumiwa wa kuwanasibisha Ma’sumiin a.s. haupo wenye ukweli, bali tunaweza kusema kuwa ni tuhuma.  Hadith hizo ni uzushi mtupu.  Katika historia ya ilimu ya Hadith, utaratibu huu mmoja ni tatizo kubwa mno kuling’amua iwapo Hadith hii ni uzushi au la.

Sayyid Murtadha ‘Alamal Hudaa a.r. anasema:

“Zipo baadhi ya sehemu za Hadith katika Mashia na Waislamu wote kwa ujumla ambazo zimejazwa makosa na uzushi ambazo zinatufanya kuzichukulia kuwa ni Hadith za uongo.

Katika Hadith hizo kuna mambo fulanifulani ambazo kwa hakika si rahisi kukubalika kiakili na ni pingamizi mtupu.  Kwa mfano imani juu ya jabr (ushurutisho) yaani mwanadamu ameshurutishwa na Allah swt katika matendo ya madhambi na uasi, au siku ya Qiyamah Allah swt ataonekana n.k. na hivyo inamaanisha kuwa kunahitajika uchuguzi na utafiti mkubwa katika kuthibitisha ukweli wa usahihi wa Hadith kama hizo.”

Imam Ali a.s. amesema: “Mtume Muhammad s.a.w.w. alisema

“Enyi watu, kumekithiri mno kuninasibishia mambo ya uzushi, hivyo mutambue kuwa mtu yeyote kwa makusudi ataninasabisha na uongo au uzushi wowote, basi hakuna mahala pale pengine isipokuwa ni Jahannam tu.”

Katika zama hizi ni lazima kufahamu ‘Ilmul Hadith na Rijal yaani kujua habari za wale wenye kuleta riwaya.  Kazi hii ni ya wale mabingwa katika fani hii na wala si ya wale wenye ilimu kidogo ambao wamejua Kiajemi na Kiarabu kidogo hivyo wakaanza kuwapotosha watu.

Sasa tuangalie ni kwa sababu gani kumetokezea haja ya kutaka kuzichuja Ahadith na tuwaangalie watu mbalimbali ambao wamefanya juhudi za kuingiza uongo na uzushi na tuhuma katika Ahadith.

(1). Baada ya kifo cha Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.  kulizuka mgogoro kuhusu ukhalifa ambapo kulitokezea makundi mawili.

Kundi moja likidai kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alikuwa amekwisha elezea ni nani atakaye kuwa Khalifa baada yake na kundi la pili likaanza kuzua Hadith kuwa swala hilo liachiwe ‘ummah wa Kiislamu kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alisema kuwa ukhalifa baada yake hautatokana na Bani Hashim (uzushi mtupu).

(2). Wakati Uthman alipouawa, basi Ma’uwiya bin abi Sufiyan kwa hila zake alitupa tuhuma za mauaji yalilengwa kwa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. Hapo kuliibuka Hadith za kuzuliwa katika kuwatukuza Bani Umayyah, umadhulumu wa Uthman na hukumu juu ya Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s.  katika mauaji ya Uthman.

Si hayo tu, bali Hadith zile zilizokuwa zikielezea fadhila za Imam Ali a.s. pia zilianza kubadilishwa na kupotoshwa.  Mfano, ipo ayah ya Qur’an tukufu: ‘wa minanaasi manyashrii nafsahubtighaa mardhatillah’ Aya hii inatoa shuhuda ya tukio lililotokea katika usiku wa Hijrah ambapo Al Imam 'Ali ibn Abi Talib  a.s.  alijitolea nafsi yake kwa ajili ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.

Kwa amri za Mu’awiyah, Hadith hii ikageuzwa kuwa imeteremka kwa ajili ya Ibn Muljim kwa sababu yeye alikuwa ameiweka nafsi yake hatarini katika kumwua Imam Ali a.s.

(3). Makhariji walizua Hadithchungumzima kuhusu akida zao na Waislamu kwa ujumla pia walizizua  Hadithnyingi mno katika upinzani wao

(4). Ma’ulamaa wa Kiislamu walianza kuzua na kutumia hizo Ahadith katika kuzieleza na kuziendeleza fikra, nadhiri na akida zao.  Mu’tazila, Tasawwuf, Gulat na Ash-Ari na wengineo wote wakaanza kuzua Hadith katika kueneza imani zao.

Iwapo utabahatika kukisoma kitabu kiitwacho Ihyaul Ulumiddiin basi ndipo utakapokuja kujua hali halisi ya uovu huu wa kuzua Ahadithza kiuongo dhidi ya Ma’sumiin a.s. ambazo kwa hakika hazikubaliki kuwa zimesemwa nao.  Kwa kutoa mfano, tunawaleteeni chache ili muweze kuziangalia:Bonyeza hapa usome zaidi

Comments (0)Add Comment

Write comment

busy
Last Updated ( Monday, 23 January 2012 19:32 )  

Vinaora Visitors Counter

mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday612
mod_vvisit_counterYesterday696
mod_vvisit_counterThis week9459
mod_vvisit_counterLast week23708
mod_vvisit_counterThis month9459
mod_vvisit_counterLast month41406
mod_vvisit_counterAll days2229577

We have: 8 guests, 2 bots online
Your IP: 54.227.49.201
 , 
Today: Mar 05, 2015

Picha za Maulamaa

 • An Image Slideshow
 • An Image Slideshow
 • An Image Slideshow
 • An Image Slideshow
 • An Image Slideshow
 • An Image Slideshow
 • An Image Slideshow
 • An Image Slideshow
 • An Image Slideshow
 • An Image Slideshow
 • An Image Slideshow
 • An Image Slideshow
 • An Image Slideshow
 • An Image Slideshow
 • An Image Slideshow
 • An Image Slideshow
 • An Image Slideshow
 • An Image Slideshow
 • An Image Slideshow
 • An Image Slideshow
 • An Image Slideshow
 • An Image Slideshow

Picha Mbalimbali

 • Slide show image
 • Slide show image
 • Slide show image
 • Slide show image
 • Slide show image
 • Slide show image
 • Slide show image
 • Slide show image
 • Slide show image
 • Slide show image
 • Slide show image
 • Slide show image
 • Slide show image
 • Slide show image
 • Slide show image
 • Slide show image
 • Slide show image
 • Slide show image
 • Slide show image
 • Slide show image
 • Slide show image
 • Slide show image
 • Slide show image
 • Slide show image
 • Slide show image
 • Slide show image
 • Slide show image
 • Slide show image
 • Slide show image
 • Slide show image
 • Slide show image
 • Slide show image
 • Slide show image
 • Slide show image
 • Slide show image
 • Slide show image
 • Slide show image
 • Slide show image
 • Slide show image
 • Slide show image
 • Slide show image
 • Slide show image
 • Slide show image
 • Slide show image
 • Slide show image

قُل هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ - Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee

Mkumbuke M/Mungu (s.w)

Kuna faida ipi ya kumkumbuka Mwenyeezi Mungu (s.w)?."Ukitaka kujua". soma zaidi

Maoni ya wasomaji wetu

Picha nzuri za Kihistoria,za Mitume na Manabii (a.
2nakuomba mwenyez mungu u2pe umri wenye manufaa nac,o wenye hasara
Sherehe za Maulid ya Kuzaliwa Kwa Mtume Muhammad (
Mjaliwe kwa kutufahamisha
Picha nzuri za Kihistoria,za Mitume na Manabii (a.
anasema sheikhul Islaam Ibn Taymiyah Rahimahullah:
Picha nzuri za Kihistoria,za Mitume na Manabii (a.
Raafidhwa

Who's on line

We have 9 guests online

Hakuna kama siku yako Ewe Husein (a.s)